CHIREMA KOMBO ATAKA WENYEJI WA KWALE KUHUSISHWA KWENYE MCHAKATO WA KUUNDA BAJETI

Madai ambayo yamekuwa yakiibuliwa kuwa wenyeji wa kaunti ya Kwale wamekuwa hawahusishwi kwenye mchakato wa kuunda bajeti yamepingwa na mwenyekiti wa kamati ya bajeti katika bunge la kaunti hiyo Chirema Kombo.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kwenye majengo ya bunge la kaunti ya Kwale Kombo ambaye pia ni mwakilishi wa wadi ya Samburu Chengoni amesema itakuwa bora ikiwa wenyeji watapewa nafasi ya kuhudhuria vikao vya umma ili kutoa mapendekezo yao.
Aidha amesisitizia umuhimu wa wenyeji kuhamasishwa kuhusiana na umuhimu wa kuhudhuria vikao vya umma vya kukusanya maoni kwani ni haki ya kila mkenya kuhusishwa kikamilifu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.