CHANJO AINA YA JOHNSON AND JOHNSON YAANZA KUTOLEWA KWA WENYEJI WA KILIFI

Idara ya afya kaunti ya Kilifi imeanza kutoa chanjo aina ya Johnson and Johnson, kwa wakazi ili kujikinga dhidi maambukizi  ya ugonjwa wa virusi vya Corona.

Kulingana na afisa wa afya ya umma katika hospitali ya rufaa ya Kilifi Erick Maitha, wamepokea dozi 500 pekee za chanjo hiyo ambayo inapeanwa mara moja.

Akizungumza  afisini mwake mjini Kilifi Maitha amesema kufikia sasa, kaunti ya Kilifi imepokea jumla ya chanjo 37,400  .

Vile vile afisa huyo amesema idadi ya maambukizi ya visa vya ugonjwa wa Corona, vinaendelea kupungua kwa kiwango kikubwa.

Aidha, Maitha amewataka wakazi wa kaunti ya Kilifi kuendelea  kufuata masharti ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19, yaliyowekwa na wizara ya afya nchini.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.