Cardiff kwenda mahakamani kupinga maamuzi ya FIFA

Klabu ya Cardiff City imetoa taarifa ya kuwa watakata rufaa juu maamuzi waliyotoa FIFA kuwa walipe Pauni Milioni 5.3 kwa klabu ya Nantes ambayo ni malipo ya awali ya usajili wa mchezaji Emiliano Sala.

Nantes walimuuza Sala kwa ada ya Pauni milioni 15 kwenda Cardiff, na timu hizo zilikubaliana malipo yafanyike katika awamu tatu.

Cardiff ambao kwa sasa wanashiriki Championship nchini England,wamesema watakata rufaa hiyo katika mahakama ya michezo duniani (CAS),Lausanne nchini Switzerland, huku wakisisitiza kuwa wana ushahidi unaoonesha kuwa usajili wa mchezaji huyo haukukamilika.

Sala,28, alifariki dunia Januari 21 katika ajali ya ndege aliyoipata wakati anasafiri kutoka Nantes kwenda Wales kukamilisha usajili wake Cardiff na kuanza kazi rasmi mwanzoni .

Taarifa ilitolewa na Cardiff City inasema
“Cardiff FC imesikitishwa sana na maamuzi ya kamati ya wachezaji (ya FIFA) iliyotoa dhidi ya klabu yetu. Tutakata rufaa CAS ili kupata maamuzi ambayo yatajali taarifa sahihi za mkataba na kutoa ufafanuzi juu ya hali yote ya kisheria kati ya klabu zote mbili.”

1 thought on “Cardiff kwenda mahakamani kupinga maamuzi ya FIFA”

  1. Pingback: Homepage

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.