BENZEMA AMNYIMA TUCHEL USHINDI

Baada ya bao la ufunguzi la Christian Pulisic dakika ya 14 ya mchezo, washindi mara 13 wa makombe ya Ulaya, Real Madrid waliambulia sare baada ya Karim Benzema kutia kimiani kunako dakika ya 29 na hivyo kufanya mechi hiyo kuisha 1-1.

Ilichukua nguvu, bidii na akili kwa mshambuliaji huyo raia wa Ufaransa kufunga bao hilo maridadi katika uwanja ya Alfredo Di Stefano usiku wa kuamkia leo na kujikumbusha kuwa bado kungali na mengi ya kupigania katika siku za usoni.

Madrid wameonyesha moto mwaka huu hususan katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Liverpool lakini siku za hivi karibuni mchezo wao umeshuka kwa sababu ya majeraha kwa baadhi ya wachezaji wao muhimu wakiwemo ; Sergio Ramos na Rafael Varane.

Thibaut Courtois , mlinda lango wa Real Madrid aliwanyima Chelsea nafasi ya kuongeza bao la pili pale alipookoa shuti la Timo Werner.

Bao la jana la Benzema linakuwa la sita la UEFA kwa mchezaji huyo msimu huu na pia la 71 katika mechi zote za michuano ya UEFA akiungana na Raul Gonzalez katika rekodi hiyo wakiwa nyuma ya Christiano Ronaldo (134), Lionel Messi (120) na Roberto Lewandoski (73).

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.