BENJAMIN TAYARI AWATAKA WAZAZI WA ENEO LA KINANGO KUTHAMINI ELIMU YA WATOTO WAO

Mbunge wa Kinango kaunti ya Kwale Benjamin Tayari ametoa wito kwa wazazi wa eneo hilo kuthamini masomo ya watoto wao.
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa madarasa ya shule za msingi za Gwasheni na Mwanda katika eneo bunge hilo, Tayari amesema hazina ya CDF kwenye kaunti ndogo hiyo imejenga zaidi ya madarasa 300 kwa kipindi cha miaka mitano.
Aidha, amewataka wazazi ambao hawana uwezo wa kuwasomesha watoto wao kutokana na ukosefu wa karo kuwachukulia Basari kutoka kwa hazina ya CDF na kaunti ili wanafunzi wao waweze kusoma bila kutatizika.
Vilevile, Tayari na wadau wengine kwenye sekta ya elimu eneo hilo wametoa himizo kwa wazazi kuhakikisha wanakuwa karibu na watoto wao kwa muda huu ambao shule zote zimefungwa kwa likizo fupi ili kupisha zoezi la uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu wa 2022.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.