Beki wa Manchester United aendelea na matibabu nchini China

Beki wa klabu ya Manchester United Diogo Dalot ambaye ameumia, amekuwa akipatiwa matibabu katika klabu ya Shanghai SIPG ya nchini China chini ya daktari wa viungo Mbrazili anayejulikana kama daktari wa miujiza.

Beki huyo Mreno mwenye umri wa miaka 20 bado hajacheza mechi yoyote msimu huu na kocha wa mashetani hao wekundu Ole Gunner Solskjaer amesema mwezi uliopita kuwa mchezaji huyo yuko nje ya uwanja hadi baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.

Dalot alitua Shanghai Agosti 29 na kutumia siku kumi pamoja na mabingwa hao wa soka wa China.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.