Aymeric Laporte awapa Manchester City kombe

Manchester City walishinda kombe la Carabao kwa mara ya nne mfululizo baada ya kuwazaba Tottenham Hotspurs 1-0 .Bao la Laporte katika dakika ya 82 liliwahakikishia wababe hao wa Ligi kuu ya Uingereza ushindi huo.

Mchezo uliomilikiwa na City kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho ,lakini cha kushangaza ilichukua dakika 82 kwa wao kupata bao la ushindi, wakiingia katika rekodi ya pamoja na Liverpool kwa kushinda mechi nane mfululizo kwenye michuano hiyo huku wakiwa wa pili kushinda michuano hiyo mara nne mfululizo baada ya Liverpool.

City wanaongoza katika Ligi kuu ya Uingereza wakiwa na alama 77 huku wakiwa na matumaini makubwa ya kubeba ligi na michuano ya mabingwa Barani Ulaya wakiwa semi fainali dhidi ya PSG , mechi itakayochezwa Jumatano ijayo.

Kipindi cha kwanza kilikuwa na presha sana baada ya Sterling kukosa nafasi nyingi za wazi za kuwaeka kifua mbele wana City huku Eric Dier akifanya kazi ya ziada kuhakikisha Sterling hangetoka na bao.

Phil Foden na Riyad Mahrez ni miongoni mwa wachezaji waliojizatiti kuonyesha uwezo wao wa kufunga bila mafanikio huku Spurs wakipata nafasi moja tu kupitia kwa Lucas Moura lakini Laporte akafanya kazi ya ziada kuzuia bao hilo.

City walisubiri hadi dakika ya 82 ambapo kupitia mpira wa ikabu uliocharangwa na Kevin De Bruyne ndipo Laporte alipata nafasi ya kufunga kwa kichwa na kuwanyanyua mashabiki 4000 katika uwanja.

City sasa wanaelekeza nguvu zao kwa EPL na UEFA watakapomenyana na PSG Jumatano ijayo katika mkondo wa kwanza huku Tottenham wakisubiria mpaka Jumapili watakapomenyana na Sheffield United.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.