ASKOFU WILFRED LAI AWARAI WAKENYA KUWACHAGUA VIONGOZI WENYE HOFU YA MUNGU

Wakenya wamehimizwa kufanya maamuzi wa busara wakati watakapokuwa wakishiriki katika uchaguzi mkuu wa agosti tisa mwaka huu wa 2022.
Kwa mujibu wa kiongozi mkuu wa dhehebu la JCC kote ulimwenguni Askofu Wilfred Lai ni kuwa hatua ya kuchagua viongozi wasio na hofu ya Mungu ndiyo chanzo cha matatizo ya taifa hili.
Akizunguza wakati wa ibada katika kanisa la JCC Bamburi, Askofu huyo amewaonya wakenya dhidi ya kuwapigia kura viongozi kwa misingi ya kikabila na badala yake kupiga kura kwa misingi ya maandiko matakatifu katika bibilia.
Wakati huohuo amewaonya wanasiasa dhidi ya kutumia dini ya kikristo ili kujitafutia umaarufu wa kisiasa na kusema  ni kinyume cha maadili ya dini hiyo na kusema  ipo haja ya waumini wa dini hiyo kujitokeza wazi na kuweka kando mizaha katika masuala yanayofungamana na dini hiyo, kama vile kuwatawaza wanasiasa kuwa mitume jambo ambalo ametaja kuwa dhihaka mbele za Mungu.

Kwa upande wake kiongozi wa dhebu la Christian Foundation Fellowship nchini Harrison Ng’ng’a,  amewahimiza waumini wa dini hiyo kujitokeza na kushiriki katika uchaguzi mkuu sio kuendelea kuomba pekee, kwani imani bila matendo imekufa.

1 thought on “ASKOFU WILFRED LAI AWARAI WAKENYA KUWACHAGUA VIONGOZI WENYE HOFU YA MUNGU”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.