ASKOFU JAMES NJIHIA ATOA WITO KWA SERIKALI KUU NA YA KAUNTI YA KILIFI KUJENGA VITUO VYA KUREKEBISHA TABIA

Askofu wa kanisa la WORLD WIDE GOSPLE CHURCH OF KENYA hapa mjini Malindi kaunti ya Kilifi James Njihia, ametoa wito kwa gavana wa kaunti ya Kilifi Gedion Maitha Mung’ro na serikali kuu kujenga kituo cha kurekebisha tabia waraibu wa dawa za kulevya katika kaunti hii.
Njihia ambaye alikuwa akizungumza na Lulu Fm kwa njia ya simu amesema licha ya kuwa kuna kituo cha Kurekebisha tabia hapa Mjini Malindi cha OMAR PROJECT bado miundomsingi yake ni duni na serikali ya kaunti ya Kilifi inapaswa kusaidia katika kuboresha kituo hicho ili kuboresha huduma za kuwanusuru waraibu wa dawa za kulevya.
Askofu Njihia amesema ikiwa kituo hicho kitajengwa kaunti ya Kilifi itakuwa afueni kwa waraibu wa dawa za kulevya kwani wengi wao hugharamika kusafiri hadi Mombasa kupata tiba.
Akizungumzia muswada wa fedha wa 2024 ambao ulitupiliwa mbali na Rais William Samoei Ruto, Askofu Njihia amesema ulikuwa umesababisha ongezeko la kodi kwenye makanisa na kutoa wito kwa uongozi wa taifa hili kuwashirikisha wadau mbambali katika kuweka mikakati ya kuboresha taifa hili kimaendeleo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *