ASILIMIA 80 YA WAGONJWA WA COVID-19 KAUNTI YA KILIFI HAWANA DALILI ZA UGONJWA HUO

Idara ya afya kaunti ya Kilifi imebaini kuwa asilimia 80 ya wagonjwa wa korona katika kaunti hii hawana dalili za wazi kuonyesha kuwa wanaugua ugonjwa huo.
Mshirikishi wa kamati ya korona ambaye pia ni afisa wa afya ya umma kaunti hii, Eric Maitha amesema kuwa imekuwa vigumu kwa wakazi kubaini iwapo wanaugua virusi vya korona au la kwa sababu wengi wao hawana dalili za ugonjwa huo ila baada ya vipimo wanapatikana kuugua ugonjwa huo.
Maitha amesema kuwa maafisa wa afya wameweka mikakati ya kuendelea kuimarisha mbinu za upimaji wa virusi hivyo kama mbinu mojawapo ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona.
Aidha afisa huyo wa afya amewataka wakaazi kuendelea kuzingatia masharti ya kudhibiti korona kwani mapuuza katika sheria hizo yamesababisha ongezeko la maambukizi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.