Asilimia 60 ya watu nchini wamepokea maji safi

Katibu msimamizi katika wizara ya maji nchini Andrew Tuimur amesema kuwa wizara ya maji nchini inashirikiana na wizara nyingine katika kuhakikisha kuwa maji ya kutosha yanapatikana shuleni kabla ya kufunguliwa baada ya kufungwa kutokana na janga la Corona.
Tuimur amesema kwamba tangu Janga hilo kushuhudiwa nchini wizara ya maji imekuwa ikishirikiana kwa karibu na wizara ya afya na ile ya elimu ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maji ya kutosha.
Katika taarifa yake huko Voi kaunti ya Taita Taveta katibu huyo amesema kuwa kufikia sasa asilimia 60 ya watu nchini wamepokea maji safi na kama wizara ya afya inapania kufikisha asilimia 100 kufikia ruwaza ya mwaka 2030.
Tuimur ameongeza kwamba mradi wa maji ya Mzima Two utaendelezwa hivi karibuni ili kuhakikisha kuwa maji ya kutosha yanapatikana hapa pwani.
Amesema mradi huo ulisimamishwa kwa muda kutokana na changamoto mbali mbali.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.