AKINA MAMA WANAOFANYA BIASHARA YA MBOGA ENEO LA MALINDI WAITAKA SERIKALI YA KAUNTI KUDUMISHA USAFI

Kina mama waliokuwa wakifanya biashara ya kuuza mboga katika kituo cha kuabiri magari hapa mjini Malindi Kaunti ya Kilifi, wamelalamika hatua ya kuhangaishwa na maafisa wa kaunti na kulazimika kutafuta eneo lipya nyuma ya soko la kwa jiwa hapa mjini Malindi ili kuendeleza bishara zao.

Wakiongozwa na Riziki Karisa wamesema wamekuwa wakihangaishwa na maafisa hao kwa mda mrefu sasa hali iliyowalazimu  kufanya uamuzi wa kusafisha eneo hilo ambalo wametakiwa kufanyia biashara kwa sasa huku wakisema wanatarajia kuimarika kwa biashara hiyo kwani hata eneo ambalo walikuwa hapo awali la kituo cha magari hawakuwa wanapata wateja wakununua mboga hizo .

Aidha sasa wanaitaka serikali ya kaunti kunadhifisha sehemu hiyo pamoja na kuwekewa hema na  mataa yatakayowasaidia wanapoendeleza biashara zao.

kwa upande wake katibu mkuu katika shirika la kutetea haki za wazee Simon Mvondi amewakashifu vikali viongozi katika eneo hili kwa kile alichokisema kuwa hawajachukua hatua zozote za kuwasaidia akina mama hao licha ya wao kujua kile wanacho pitia.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.