AFCON | Nigeria na Senegal zafuzu nusu fainali, Afrika Kusini na Benin zatemwa nje

Timu ya taifa ya Nigeria, Super Eagles imetinga nusu fainali baada ya kuilaza Afrika kusini kwa magoli mawili kwa moja kwenye mechi yao ya robo fainali ya michuano ya kombe la mataifa bara Afrika inayoendelea nchini Misri.

William Troost-Ekong alifunga goli la dakika za mwisho na kuisaidia Nigeria kutinga nusu fainali ya kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Afrika Kusini.

Samuel Chukwueze alifunga goli la kwanza la Nigeria baada ya kupata krosi nzuri kutoka kwka Alexi Iwobi kabla ya kufunga baada ya jaribio la pili.

Hatahivyo Bongani Zungu alisawazisha kupitia kichwa kilichodaiwa kuwa cha kuotea kabla ya refa wa Video VAR kusema kwamba mpira huo ulikuwa umemgonga mchezaji wa Nigeria kabla ya kumfikia.

Lakini mchezaji wa Udeneese Troost-Ekong alifika katika lango la Afrika Kusini katika muda uliotarajiwa na kuweza kucheka na wavu na hivyobasi kuisadia timu yake kufusu nusu fainali.

Kwa upande wa mechi nyengine ya robo fainali ambayo imewakutanisha Simba wa Teranga, Senegal na timu ya taifa la Benin ni kwamba Benin wameshindwa kufuzu nusu fainali kwa kuruhusu bao moja bila jawabu dhidi ya Simba hao na kutemwa nje ya michuano hiyo ya Afcon.

Gueye alitamba na mpira na kumpigia pasi nyota wa Liverpool Sadio Mane ambaye hakuwa mchoyo akaamua kumrudishia ambapo mchezaji huyo alicheka na wavu.

Refa wa kutumia kanda ya video VAR amezinduliwa katika awamu ya robo fainli ya michuano hiyo hivyobasi Mane alikuwa na magoli mawili ambayo yalikataliwa kwa kuotea.

Mchezaji wa Benin Olivier Verdon alipigwa kadi nyekundu baada ya kumchezea visivyo Gueye.

Kabla ya goli la Gueye, ambalo ni lake la kwanza nchini Misri , Benini ambayo ilitinga hadi robo fainali bila ya kushinda mechi katika dakika 90 karibu ichukue uongozi baada ya masikhara ya mlinda lango Alfred Gomis.

Kipa huyo alishindwa kudhibiti pasi aliopigiwa na mchezaji mwenzake kabla ya mpira huo kutoka nje.

Na sasa Nigeria itacheza dhidi ya Ivory Coast au Algeria siku ya Jumapili katika nusu fainali ya pili.

Super Eagles walipata ushindi wa halali na kuongoza kupitia mchezaji wa Villarreal Chukwueze.

Wangeongeza magoli zaidi wakati Williams alipopangua shambulio la Peter Etebo lililopiga chuma cha goli na kutoka nje.

Goli la Zungu lilikuwa la kwanza katika michuano hiyo ya Afrika kukubalia na refa wa VAR.

Goli hilo lilionekana kuwa la kuotea lakini mwaju wa adhabu wa Percy Tau ulimgonga Odion Ighalo kabla ya kumfikia ambapo Zungu alifunga kwa kutumia kichwa.

Senegal itakumbukwa na Afrika mashariki baada ya kuwalima Kenya, Tanzania na Uganda na kuwasababishia majanga ya kutemwa nje ya michuano hiyo.

Simba wa Teranga walikung’uta Tanzania magoli mawili kwa nunge kwenye mechi yao ya kwanza kabla ya kuwafunganishia virago Kenya kwa kuwalima magoli matatu bila jawabu kwenye hatua ya makundi kisha kuwazamishia mashua Uganda kwa goli moja sifuri kwenye hatua ya muondoano ya 16 bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.