AC Milan yaajiri kocha mpya saa chache baada ya kumuachisha kazi Marco Giampalo

Bingwa wa Italia AC Milan imemtaja mrithi wa kocha Giampalo, atakaechukua nafasi ya ukufunzi huku akipewa kandarasi ya hadi Juni 2021.

Milan imemuandikisha kandarasi Stefano Pioli mwenye umri wa miaka 53 mda mfupi baada ya kumuachisha kazi Marco Giampalo jana Jumanne kufuatia kuandikisha matokeo duni ya mapema msimu huu wa 2019/2020.

Klabu hiyo kwa sasa inashikilia nafasi ya 13 kwenye jedwali la ligi ya Serie A ikiwa na alama 9 hiyo ikiwa ni alama kumi nyuma ya Juventus wanaoshikilia bendera ya ligi hiyo huku nafasi ya pili na tatu Inter Milan na Atlanta mtawalia.

Milan itakuwa mwenyeji wa mechi yao inayofuata dhidi ya Leece baada ya pumziko la kupisha michuano ya kimataifa ya Euro 2020.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.