GAVANA MWADIME ASEMA MCHAKATO UMEANZISHWA KUDHIBITI UHABA WA MAJI TAITA TAVETA

Serikali ya kaunti ya Taita Taveta imeanzisha mchakato wa kutafuta wafadhili kutoka mataifa mbalimbali, kuwasaidia kukabiliana na changamoto ya uhaba wa maji kwenye kaunti hiyo.
Akizungumza katika taifa la Dubai, gavana wa kaunti hiyo Andrew Mwadime, amesema  iwapo tatizo hilo litapata suluhu la kudumu, wananchi wengi watapata afueni ya madhila wanayokumbana nayo kusaka maji.
Kulingana na gavana huyo, mojawapo ya suluhu la tatizo hilo ni utunzi wa misitu ya kaunti hiyo ambayo itasaidia katika kuleta mvua..
Kwa upande wake waziri wa maji kaunti hiyo Granton Mwandawiro, amesema licha ya kaunti hiyo, kuwa na vyanzo vya maji na rasilimali nyingine nyingi, wameshindwa kusambaza bidhaa hiyo kwa wananchi wa kaunti hiyo, kutokana na kiasi kidogo cha fedha wananchopokea, kutoka kwa serikali ya kitaifa na kusema  kuwa shilingi bilioni 18.5, zitatosha kutatua changamoto hiyo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *