MBUNGE WA MVITA ABDULSWAMAD SHARIFF NASSIR ANZISHA MPANGO WA KUBORESHA MASOMO KAUNTI YA MOMBASA

Siku chache baada ya wizara ya elimu nchini kutangaza matokeo ya mtihani wa KCPE, matokeo ya somo la Kiswahili katika shule mbali mbali  eneo bunge la Mvita, yametajwa kurudi chini ikilinganisha na matokeo  ya somo la kiingereza mwaka huu.

Akizingumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa matokeo ya mtihani wa mwaka wa 2020, katika ukumbi wa shule ya upili ya Star Of The Sea  kwa watahiniwa wa shule za msingi, zilizopo ndani ya eneo bunge la Mvita, Mbunge wa mvita Abdulswamad Shariff Nassir, amesema licha ya kuwa ukanda wa Pwani ndio chimbuko la lugha ya Kiswahili,  kuna haja ya wanafunzi kuzingatia zaidi  lugha hio,  akitaja mchanganyiko wa lahaja tofauti tofauti hapa Pwani, kama miongoni mwa sababu zinazopelekea somo la kiswahili kurudi chini.

Somo la Kiswhili lilikuwa na jumla ya alama 52.83, huku lile la Kiingereza likiwa na jumla ya alama 61.92, katika shule za gatuzi dogo la  Mvita kaunti ya mombasa.

Aidha Abdulswamad amesema anapania kuendeleza mradi wa kusambaza vitabu vya marudio kaunti ya Mombasa,  katika shule mbali mbali kama njia moja wapo ya kuinua kiwango cha elimu zaidi hapa Pwani.

Wakati huo huo naibu kamishna gatuzi dogo la Mvita Robin, Ngeiwo (D.O 1) amesisitiza haja ya kujiunga na shule za upili, kwa  wanatahiniwa wote waliomaliza darasa la nane pasi na kisizingio cha karo, ili kuafikia asilimia 100 ya wanafunzi  watakao kujiunga na masomo ya sekondari.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.