IDADI YA WATU WANAOUGUA MALARIA ENEO LA PWANI YA SEMEKANA KUPUNGUA KWA KIASI KIKUBWA

Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya malaria hapo jana,imebainika kuwa wagonjwa wanaougua malaria katika ukanda wa pwani wamepungua kwa kiasi kikubwa sambamba na vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku hiyo,katibu msaidizi katika wizara ya afya,Rashid Aman amesema kuwa Kenya pia imejizatiti katika kuzuia athari za malaria kupitia kugawanya vyandarua vya kujikinga dhidi ya ugonjwa huo sawia na kutoa hamasa kwa umma kuhusiana na mbinu za kuepuka malaria.

Aman amesema kuwa kwa sasa wanaogua ugonjwa huo wamekuwa wachache mno kinyume na hali ilivyokuwa miaka ya hapo nyuma kwani kwa sasa kati ya watu 1000 ni 86 pekee ndio wanaougua ugonjwa wa malaria.

Aidha katibu huyo amesema kuwa ipo haja ya wataalamu wa afya kwa ushirikiano na wizara ya afya, kuchukua hatua ya kuhakikisha kuwa wanahamasisha jamii kuhusiana na jinsi, ya kujikinga dhidi ya maradhi hayo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.