ZOEZI LA USAJILI WA MAKURUTU KWENYE IDARA YA POLISI LAZIDI KUKASHIFIWA

Baadhi ya wakaazi mjini Malindi kaunti ya Kilifi walioshiriki katika shughuli ya usajili wa maafisa wa Polisi uwanjani Alaskan hapo jana wameelezea kugadhabishwa kwao na jinsi shughuli hiyo ilivyoendeshwa, wakisema haikuwa ya huru na haki.

Wakiongozwa na Mercy Karisa na Gideon Tsuma, wanadai zoezi hilo limekuwa na udanganyifu kwani licha ya kuafikia vigezo hitajika, bado hawakuweza kusajiliwa.

Aidha, wanadai maafisa wakuu wasimamizi hawakuwaeleza sababu zilizochangia kwa wao kuachwa nje kwenye shughuli hiyo.

Mkaazi wa mtaa wa Kasufini mjini humo Charo John aliyeshuhudia shughuli hiyo, amedai ingekuwa haki kama nafasi za jinsia ya kike zingeongezwa badala ya kuwekwa mbili pekee.

Hata hivyo, Afisa mkuu msimamizi wa shughuli hiyo mjini Malindi Eliud Monari, ameeleza kwamba waliofanikiwa kwenye usajili huo walifaa kuwa na vyeti hitajika.

Monari amebainisha kwamba, kwenye shughuli hiyo wamesajili jumla ya vijana 21 ambapo wasichana wawili pekee ndio wamefanikiwa kusajiliwa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.