Zoezi la ununuzi wa chakula cha msaada kuanzishwa lamu

Serikali ya kaunti ya Lamu inapania kunzisha zoezi la ununuzi wa chakula cha msaada punde tu fedha zilizotengewa shughuli hiyo zitakapoidhinishwa na bunge la Kaunti hiyo.
Gavana wa kaunti hiyo Fahim Yassin Twaha amesema kulingana na sheria kama serikali ya kaunti hawana ruhusa ya kutumia fedha za umma bila idhini ya bunge la kaunti hiyo.
Kulingana na Fahim ni kuwa zoezi hilo litakapong’oa nanga litawalenga wenyeji ambao hawana uwezo huku akiwataka kuzingatia maagizo yanayotolewa na serikali kupitia wizara ya afya katika kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.