ZOEZI LA KUPEANA DAWA ZA KICHOCHO LIMEANZISHWA KAUNTI YA KILIFI

Serikali ya Kaunti ya Kilifi imeanza rasmi zoezi la kupeana dawa za Kichocho kwa wakazi wa Kaunti ya Kilifi.

Kulingana na afisa mkuu wa magonjwa yaliyotolekezwa Patrick Makazi ni kuwa ugonjwa wa Kichocho unasababishwa na viini vinavyo patikana ndani ya maji ya vidimbwi ama mabwawa na huathiri pakubwa sehemu ya kibofu cha mkojo.

Makazi amesema watoto wadogo ndio walio katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa kichocho.

Aidha amesema dawa hizo zinalenga Wakazi wote isipokuwa watoto walioko chini ya miaka minne hivyo basi kuwataka wakazi wote kumeza tembe hizo ili kujikinga na ugonjwa huo.

Ameongeza kuwa tayari madaktari wa nyanjani wameanza kupeana dawa hizo na huenda takribani wadi ishirini zikafikiwa na dawa hizo.

Zoezi hilo litachukua takriban siku sita na limeratibiwa kutamatika siku ya jumapili.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.