ZOEZI LA KUKUSANYA SAINI LAZINDULIWA RASMI KAUNTI YA KWALE

Zoezi la kukusanya saini za kuunga mkono ripoti BBI limezinduliwa rasmi na gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya.
Akizindua rasmi shughuli hiyo huko Ukunda Gavana huyo amewataka wenyeji ambao wanaipinga ripoti kuiunga mkono kwa madai itaongeza idadi ya maeneo bunge kaunti hiyo na kuwataka kuisoma na kuielewa vyema kabla ya kufanya maamuzi yao dhidi ya ripoti hiyo.
Ameongeza kwamba ni ripoti ambayo itawaunganisha wakenya sambamba na kutatua ghasia za baada ya uchaguzi nchini ambazo zimekuwa zikishuhudiwa baada ya maandalizi hayo.
Naye Kamishna wa kaunti hiyo Karuku Ngumo amesema kuwa wanapania kukusanya sahihi laki 1 katika kaunti hiyo na tayari kufikia sasa zaidi watu elfu 10 wametia saini na zoezi hilo limeratibiwa kutamatika leo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.