ZIARA YA KUTATHMINI IDADI YA WANAFUNZI WALIO RUDI SHULE KATIKA MSITU WA BONI KAUNTI YA LAMU YAANDALIWA

Maafisa wa serikali na wale wa wizara ya elimu wamefanya ziara katika shule zilizoko kwenye msitu wa Boni kaunti ya Lamu kutathmini hali ya masomo kwa wanafunzi waliorejea hadi sasa huku hali ngumu ya maisha kwenye shule hizo ikisemekana kuwakabili kwa wanafunzi hao.

Wanafunzi hao katika shule ya msingi ya Mararani wanadaiwa kukumbwa na ukosefu wa viatu na sare za shule kutokana na hali ya umaskini unaowakabili wakaazi wao.

Wanafunzi wanaosomea kwenye shule zilizoko kwenye msitu wa Boni ni wanafunzi wa chekechea pamoja na wale darasa la nne kwani wanafunzi wengine walihamishiwa hadi shule zingine za bweni.

Katibu wa kuhudumu katika biashara na viwanda nchini, Jonstone Mweru amezuru maeneo hayo ili kujua changamoto za wakaazi huku akiwapongeza kwa kuwapeleka watoto wao shuleni.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.