Werner na Havertz ‘waanza kazi’ kwa kuandikisha ushindi

Sajili mpya Timo Werner na Kai Havertz ambao walijiunga na Chelsea msimu huu wameanza vyema kwenye kipute cha ligi kuu ya Uingereza EPL kwa kuwasaidia waajiri wao kunyakua ushindi wa magoli 3-1 ugenini usiku wa kuamkia leo katika dimba la Amex dhidi ya Brighton.

Hakim Ziyech na Ben Chilwell walikosa mechi hiyo kwa sababu ya jereha huku Thiago Silva pia akkikosekana. Frank Lampard hata hivyo, alibuni kikosi imara kwa mchezo huo kwa kuwashirikisha Werner na Havertz kuongoza timu ya kwanza. 

Werner ndiye alikuwa kifaa bora huku nyota huyo wa Ujerumani akitunukiwa matuta ya penalti katika dakika ya 23 ambayo Jorginho alichonga ndizi hadi kimyani na kuwaweka kifua mbele.

Hata hivyo, wenyeji walisawazisha bao hilo dakika 10 kabla ya awamu ya pili kupitia kwa Leandro Trossard ambaye alivurumisha kombora kali lililompita Kepa Arrizabalaga kutokea yadi 22.

Reece James aliendeleza uongozi wa Chelsea dakika chache baadaye kwa kufunga bao tamu la ufundi. Kurt Zouma aliweka mchezo huo kwenye kilele chake kunako dakika ya 66, ambapo juhudi zake zilimsaidia kutingisha wavu.

Wenyeji hao wa London hatimaye walitwaa ushindi wa 3-1 na kujiunga na vilabu vingine kama vile Arsenal na Liverpool ambao walifungua kampeni zao kwa ushindi.

Aidha kwenye mechi ya awali, Sheffield United walilalia kipigo cha goli 1 kwa sifuri dhidi ya wageni Wolves.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.