WENYEJI WA PWANI WATAKIWA KUCHUKUA KADI ZAO ZA HUDUMA NAMBA

Afisa mkuu wa usajili wa watu kanda ya pwani Agrey Masai amewataka wenyeji wa ukanda huu kuchukua kadi zao za huduma Namba.

Masai amesema kwamba kuna zaidi ya kadi elfu 51 za huduma Namba ambazo hazijachukuliwa katika afisi hizo.

Ameongeza kuwa pwani wamepokea zaidi ya kadi elfu 57 kufikia sasa huku zile ambazo zimechukuliwa zikiwa elfu 5 pekee na kusema kadi hizo ziko tayari hivyo wakenya wanapaswa kuzichukua katika ofisi husika kanda ya pwani.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.