Wenyeji wa Mararani Lamu waomba msaada wa chakula

Serikali ya kaunti ya Lamu imetakiwa kuwapa wenyeji msaada wa chakula kutokana na hali ngumu ambayo imechangiwa na janga la Corona ambalo linaendelea kushuhudiwa nchini na ulimwenguni kwa ujumla.
Kulingana na balozi wa nyumba kumi eneo la Mararani Jesicah Ngoa amesema kwamba wenyeji wa kaunti hiyo hawana namna ya kujitafutia mapato baada ya shughuli nyingi kuathiri na mlipuko wa COVID-19.
Baadhi ya wenyeji hao wamekuwa wakifanya vibarua katika hoteli za kitalii wadi ya Shella ambazo zimefungwa na kwa sasa hawawezi kulipa kodi za nyumba zao kutokana na hali hiyo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.