Wenyeji wa lamu waonywa dhidi ya kubeba panga na visu

 

Wenyeji wa kaunti ya Lamu wameonywa dhidi ya kubeba panga ua kisu katika kaunti hiyo.
Haya ni kulingana na kamishna wa kaunti hiyo Irungu Macharia ambaye amehoji kuwa baadhi ya vijana wamekuwa wakitumia silaha hizo katika kutekeleza uhalifu.
Kulingana na Macharia ni kuwa hadi kufikia sasa visa vya wizi wa kimabavu vimeongezeka kwa kiwango kikubwa katika kaunti ya Lamu na kuwaonya wanaotekeleza uhalifu kuwa watakabiliwa kwa mujibu wa sheria.
Macharia amewahimiza viongozi wa kisiasa, wa kidini sambamba na wa Kijamii kutafuta mbinu za kutatua mizozo katika jamii ili kudhibiti visa hivyo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.