Wenyeji wa Kwale watakiwa kuzingatia tahadhari ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona

Wenyeji wa kaunti ya Kwale wametakiwa kupiga ripoti kwa maafisa wa afya kupitia nambari ya 988 ikiwa watashuhudia mtu yeyote mwenye dalili za virusi vya Corona.
Haya ni kulingana na kamishna wa kaunti ya Kwale Karuku Ngumo ambaye amesema agizo la watu kukaa nyumbani linapaswa kutekelezwa kwani kwa kiwango kikubwa litasaidia kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo.
Amesema kila mmoja anafaa kuzingatia tahadhari hiyo ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona katika kaunti hiyo na taifa la Kenya kwa ujumla.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amesema kuwa baadhi ya viongozi wa kidini ambao wamekaidi amri ya serikali za kuzifunga nyumba za ibada kuwa watakabiliwa kwa mujibu wa sheria.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.