Wenyeji wa Vanga wanaojihusisha na upanzi wa mikoko wapata msaada wa Chakula

 

Wakaazi wa Vanga kaunti ya Kwale wanaojihushia na upanzi wa misitu ya mikoko wamenufaika na msaada wa chakula kutoka kwa taasisi ya utafiti wa bahari Kenya Marine and Institute Research.
Wakiongozwa Zulekha Hassan wakaazi hao wamehoji kuwa wapo watu katika jamii ya eneo hilo ambao wameathirika pakubwa baada ya mipaka ya taifa la Tanzania kufungwa kufuatia mkurupuko wa maambukizi ya Covid 19 ikiwemo wavuvi wanaotegemea kazi hiyo kupata kipato chao cha kila siku.
Wavuvi hao pia wamekiri kupungua kwa mapato yao tangia chimbuko la ugonjwa wa covid 19 jambo lililowapelekea kuitisha msaada wa dharura wa chakula na mahitaji mengine ya kimsingi

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.