Zoezi la kugawanya vyandarua vya kuzuia mbu kwa wenyeji wa kaunti ya Kwale linatarajiwa kuanzishwa na wizara ya afya katika kaunti hiyo ili kudhibiti ugonjwa wa Malaria.
Kulingana na afisa ambaye anasimamia ugonjwa wa Malaria katika kaunti hiyo Elizabeth Chomba amehoji kuwa majadiliano yanaendelezwa na wadau mbali mbali wa afya ili kuhakisha shughuli hiyo inafanikishwa.
Wakati uo huo ameongeza kuwa wenyeji watalazimika kubeba vitambulisho ili kusajiliwa huku akiwataka kujitokeza kwa wingi.