WAZEE WAKAYA MJINI MALINDI KAUNTI YA KILIFI WA ANZISHA MPANGO WA KUHUBIRI AMANI ENEO HILO

Mwenyekiti wa muungano wa Malindi District Cultural Association Emmanuel Munyaya amesema Wazee wa Kaya mjini Malindi kaunti ya Kilifi, wanalenga kufanya matembezi ya kilomita 68 kwa muda wa siku nne lengo kuu likiwa ni kuhubiri amani katika jamii.

Munyaya amesema pia watahamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutunza wazee badala ya kuwauwa kwa tuhuma za uchawi na kupitia matembezi hayo jamii itapata fursa ya kuhamasishwa masuala yanayowahusu pamoja na kuenzi utamaduni.

Kwa upande wake katibu wa muungano huo Joseph Karisa Mwarandu, anasema  baada ya matembezi hayo watafanya kongamano kujadili kuhusu kununuliwa kwa ardhi ya Shakahola ambako shujaa Mekatilili wa Menza alimpiga kofi mkoloni.

Mzee Mwarandu pia amewahimiza wadau wa sekta tofauti kushirikiana ili kufanikisha mpango huo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.