WAZAZI WATAKIWA KUCHUNGUZA FILAMU NA VIDEO WANAZOTIZAMA WATOTO WAO KWENYE RUNINGA

Sharti wazazi wachukue jukumu la kufuatilia kwa ukaribu vipindi na filamu wanazozitazama watoto wao pale wanapokuwa majumbani ama hata sehemu nyingine.

Haya ni kwa mujibu wa msimamizi mkuu wa bodi ya kudhibiti filamu KFCB katika eneo la Pwani Bonventures Kioko ambaye amehoji kuwa zipo baadhi ya programu ambazo wazazi hulipia katika runinga ambazo bado hazijathibitishwa na bodi ya filamu humu chini na hivyo basi kuvipeperusha vipindi ambavyo havina maadili kwa watoto.

Hata hivyo Kioko amesema kuwa bodi hiyo imekuwa ikipiga marufuku baadhi ya filamu na video za wakenya kwa kile alichokisema kuwa ni moja wapo ya mambo yanayochangia kutokuwepo kwa maadili kwa watoto katika jamii.

Aidha amewataka wananchi kuchukua jukumu la kutaka kujua umuhimu wa vipindi na video wanavyovitazama huku akimkashifu vikali mchekeshaji maarufu nchini Eric Omondi kwa kupeperusha vipindi visivyo na maadili katika jamii.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.