Wazazi Lamu watakiwa kujukumikia watoto

Naibu mkurugenzi katika idara ya elimu kaunti ya Lamu Bi Rukia Abdalla amewataka wazazi katika kaunti hiyo kuwapa watoto wa kike mahitaji ya msingi wakati huu ambapo wako majumbani kutokana na janga la Corona.
Amesema wakati huu ambapo shule zimefungwa wanafunzi wa kike wanakosa kunufaika na mradi kutoka kwa wizara ya elimu hivyo wazazi wanapaswa kujukumika kama inavyopaswa.
Kulingana na naibu mkurugenzi huyo ni kuwa huenda watoto wengi wa kike katika kaunti hiyo wakapata mimba za utotoni na kukatiza masomo yao ikiwa wazazi watakosa kuwajibikia majukumu yao.
Haya yanajiri huku visa vya dhuluma dhidi ya watoto vikiendelea kuongezeka katika kaunti mbali mbali nchini.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.