WAZAZI ENEO BUNGE LA MAGARINI WATAKIWA KUWAJUKUMIKIA WATOTO WAO

Baadhi ya wazazi katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi wamekosa kujukumika kama inavyopaswa katika jitihada za kuwalipia karo ya shule kufuatia hatua ya wengi wao kutegemea kilimo ambacho kimekuwa kikiwapa mapato ya chini.
Haya ni kwa mujibu wa mweyekiti wa hazina ya CDF katika eneo bunge hilo Samson Kombe ambaye amehoji kuwa licha ya mapato yanayotokana na kilimo kudorora wapo baadhi yao ambao wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha watoto wao wanalipiwa karo ya shule.
Kombe amewanyooshea kidole cha lawama machifu katika eneo hilo kwa madai ya kuwapeleka baadhi ya wanafunzi katika shule zingine bila kutoa taarifa kwa ofisi husika hali ambayo imechangia kwa wanafunzi wengi kufukuzwa shule kutokana na ukosefu wa karo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.