Wawakilishi wa kike kaunti ya kilifi kuanzisha kuanzisha hamasa kwa watoto wa kike kuhusu athari za kushiriki ngono za mapema

Kampeni ya kuhamasisha watoto wa kike kuhusu athari za kushiriki ngono za mapema zinatarajiwa kufanywa na wawakilishi wa kike katika kaunti kwenye kaunti ya Kilifi
Haya ni kwa mujibu wa Mwakilishi wa wadi ya Magarini kaunti ya Kilifi Elina Mbaru ambaye amesema mpango huo unajiri baada ya kubainika kwamba Kilifi ni miongoni mwa maeneo yanayoongoza kwa visa vya mimba na ndoa za mapema nchini.
Kulingana na Elina Mbaru ni kuwa kupitia hamasa hizo wanafunzi wa kike kaunti ya Kilifi watajiepusha na masuala ya dhulma za kijinsia.
Wakati huo huo amewahimiza washikadau kushirikiana katika jitihada za kufanikisha mpango huo huku akiwataka mahakimu katika mahakama ya Malindi kuhakikisha wanazuru shule mbali mbali ili kusistizia suala hilo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.