Wauguzi Tana River watishia kuandaa mgomo

 

Katibu wa chama cha wauguzi tawi la Tana River kaunti ya Tana River Damon Kwaraa amesema huenda wahudumu wa afya katika hospitali ya rufaa ya Hola katika kaunti hiyo wakagoma ikiwa serikali ya Tana River itakosa kusikiza lalama zao kutokana na changamoto zinazowakumba.
Kwaraa amesema kwamba baadhi ya idara katika wizara ya afya huko Tana River zinasimamiwa na watu ambao hawajahitimu hali ambayo inatia wasi wasi kwani iwapo hazitachukuliwa hatua za haraka huenda kukashuhudiwa madhara.
Amesema kwamba kuna uhaba wa vyoo vya wahudumu wa afya na ni hali ambayo imekuwa ikiwalazimu kujisaidia nyumbani na kusema ni jukumu la serikali kuhakisha mazingira ya kufanyia kazi yako sawa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.