Wauguzi na Madaktari kwenye hospitali ya kaunti ndogo ya Malindi wapokea vifaa vya kujikinga dhidi ya Corona

 

Shirika la kutetea haki za binadamu la MUHURI mkoa Wa pwani limetoa msaada wa vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona kwa wauguzi na madaktari katika hospitali ya kaunti ndogo ya Malindi kaunti ya Kilifi.
Akizungumza na wanahabiri katika zoezi la kupeana vifaa hivyo kwenye hospitali hiyo afisaa mkuu Wa nyanjani katika shirika hilo Bi Afie Swale amesema kuwa shirika hilo lilipokea vifaa hivyo kutoka kwa wafadhili wao ili kupeana katika baadhi ya hospitali zilizoko kanda ya pwani. 
Bi swale ameongezea kuwa licha ya serikali ya kaunti kutoa bidhaa hizo bado kuna uhutaji wa vifaa hivyo ili kutumika katika shughuli mbali mbali.
Aidha, Evans Nyambogwa msimamizi wa hospitali hiyo amethibitisha kupokea msaada huo  na kusema kuwa utawasaidia kupiga hatua huku wakingojea serikali kutoa mchango wake kwani janga la Corona halikuwa limeratibiwa katika bajeti ya mwaka hivyo basi ni jambo la busara kwa mashirika kutoa misaada hiyo

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.