Watu 80 wathibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona

Kwa mara ya kwanza kwa muda wa saa 24 taifa la Kenya limerekodi idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona baada ya watu 80 kuthibitishwa kuambukizwa virusi hivyo na kufikisha jumla ya watu 1109.
Katika taarifa yake alipokuwa anatoa takwimu kuhusiana na Covid-19 waziri wa afya nchini Mutahi Kagwe amesema idadi hiyo imeshuhudiwa baada ya sampuli 3102 kufanyiwa uchunguzi.
Waziri huyo amesema kati ya visa hivyo 80 watu 41 ni kutoka kaunti ya Nairobi, Mombasa 20 na 7 kaunti ya Siaya.
Wakati uo huo ameongeza kuwa 7 hao wanadaiwa kuambukizwa baada ya kusafiri kutoka Kibra kaunti ya Nairobi ili kuhudhuria mazishi bila kuzingatia sheria za serikali.
Hata hivyo, amethibitisha watu 9 wamepona Covid-19 na kuruhusiwa kwenda nyumbani huku idadi ya waliopona nchini ikifikia 375 na waliofariki ikisalia 50.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.