Watu 39 zaidi waruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupona Corona

 

Waziri wa Afya nchini Mutahi Kagwe amesema Kenya ingali katika hatari ya kupata maambukizi zaidi ya virusi vya Corona siku za usoni kama inavyoshuhudiwa katika mataifa mengine nchini.
Akihutu katika majengo ya wizara ya Afya Kagwe amesema zoezi la kupima halaiki ya watu limebainisha jinsi virusi hivyo vimeenea kutokana na idadi kubwa ya visa vinavyorekodiwa.
Akitoa takwimu Kagwe ametangaza maambukizi mengine 124 mapya ambayo yamerekodiwa katika saa 24 zilizopita baada ya sampuli 2640 kufanyiwa vipimo na idadi kufikia 2,340.
Watu 39 zaidi wamepata nafuu na kuondoka hospitalini huku sasa jumla ya waliopona kutokana na virusi hivyo ikifika 592.
wagonjwa wengine 4 wamepoteza maisha yao kutokana na virusi hivyo hatari na idadi kufikia 78.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.