WASIMAMIZI WA SHULE KAUNTI YA KILIFI WAHIMIZWA KUIMARISHA USALAMA KWA WANAFUNZI WANAPOKUWA SHULENI

Wazee wa nyumba kumi eneo la Mnarani, kaunti ya Kilifi wamewataka wasimamizi wa shule kuwa makini zaidi ili kuhakikisha usalama wa wanafunzi wanapokuwa shuleni.

Wakiongozwa na Lennox Chiringa wamesema kuwa kuna haja ya usalama kuimarishwa katika mazingira ya shule ili kuona kwamba wanafunzi wanaendeleza shughuli za masomo bila kutatizika.

Chiringa ameyasema haya akirejelea kisa ambapo mwanafunzi mmoja wa darasa la tano katika shule moja ya kibinafsi eneo la Ganze kaunti ya Kilifi aliponea jaribio la utekaji nyara.

Kulingana na mwanafunzi huyo kwa jina Eric Kombe jamaa huyo aliyeazimia kumteka nyara alimhadaa kuwa anahitaji usaidizi kabla ya kumuingiza ndani ya gari alilokuwa akiendesha na kusafiri naye kutoka Ganze hadi mjini Kilifi.

Hatahivyo wazee wa mtaa kule mnarani walifanikiwa kumkutanisha motto huyo na babu yake ambaye alimchukua na kwenda naye nyumbani.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.