Wapwani wengi wataathirika endapo suala la SGR halitapata utatuzi wa haraka, asema mbunge wa Mvita

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir amesema biashara nyingi kwa sasa zimefungwa na zingine kuzorota huku idadi kubwa ya wakaazi wa Mombasa wakiachwa bila ajira baada ya kupoteza ajira katika baadhi ya kampuni za uchukuzi walizokuwa wakifanyia kazi.

Nassir amesema kuwa hali hii imepelekewa na amri ya serikali ya kusafirisha makasha kutoka bandari ya Mombasa kupitia reli mpya ya kisasa.

Mbunge huyo amesema kuwa atazidi kuungana na mashirika mbalimbali na washidau wa sekta ya uchukuzi kaunti ya Mombasa ili kuona kwamba wanautetea uchumi wa kaunti hiyo sambamba na ajira kwa wakaazi wa pwani.

Swamad ameongeza kuwa wapwani wengi wataathirika endapo suala hilo halitapata utatuzi wa haraka kupitia serikali ya kitaifa.

Aidha hapo jana vuguvugu la okoa Mombasa kupitia katibu muandalizi wa shirika la first action business community movement, Harriet Muganda limetishia kufanya maandamano ya kila siku ili kuhakikisha kuwa wakaazi wa pwani wamepata haki

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.