Wanawake wanaofanya biashara ya ngono mjini Malindi walalamikia kudorora kwa biashara hiyo.

 

Wanawake wanaofanya biashara ya ngono mjini Malindi kaunti ya Kilifi wanalalamikia kuhangaishwa na idara ya polisi kwa sababu walizozitaja kama zisizokuwa na msingi.
Wakiongea na mwanabari wetu, wauza ngono hao wamedai kuhangaishwa na polisi kwa shutuma za kukiuka masharti ya kafyu ila kulingana na wao maafisa wa polisi wamekuwa wakiwapiga hata wakiwa majumbani huku wengine wakiishia kukamatwa na kufikishwa korokoroni.
Kwa sasa baadhi yao wanauguza majeraha kutokana na kipigo hicho kutoka kwa maafisa hao wa polisi.
Aidha, Machangudoa hao wamedai kuwa maafisa hao huwaitisha hongo kila wakati na kuwatishia kuwapeleka korokoroni huku wakidai kuwa wao wanafanya biashara ya ngono ili kukimu mahitaji ya familia zao.
Makahaba hao wamedai kutengwa na serikali ya kaunti katika ugavi wa chakula cha msaada wakati huu wa janga la korona huku wakielekezea maafisa tawala kidole cha lawama.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.