Wanaoishi karibu na mto Tana watahadharishwa

Wenyeji katika kauti ya Lamu wanaoishi karibu na mto Tana ambao umevujunja kingo zake wanaendelea kuhimizwa na viongozi wao kuhamia maeneo salama ili kuepukana na mafuriko.
Wakiongozwa na mbunge wa Lamu Magharibi Stanley Muthama amesema sehemu za Chalaluma, Dide Waride na Moa ni maeneo ambayo yanapakana na Mto Tana na wanapaswa kuhamia maeneo salama ili kuepukana na maafa.
Wakati uo huo gavana wa kaunti hiyo Fahim Yassin Twaha amepiga jeki kauli hiyo na kuwataka kuchukua tahadhari kutokana na mvua kubwa ambayo inaendelea kushuhudiwa kaunti hiyo.
Kufikia sasa zaidi ya nyumba 600 zimesombwa na mafuriko ya maji yaliyotoka nyanda za juu na kupelekea mto Tana Kufurika.
#

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.