WALIMU NA WANAFUNZI WA SHULE ZA UPILI NA MSINGI HUKO KALOLENI WAKABIDHIWA BARAKOA

Shirika moja lisilo la kiserikali limewakabidhi Walimu wakuu wa shule za msingi na upili katika eneo la Kaloleni kaunti ya Kilifi barakoa

zitakazosambazwa kwa wanafunzi wa shule hizo ili kuwakinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Akizungumza katika eneo la Kizurini, mwenyekiti wa muungano wa wazazi kaunti ya Kilifi Juma Khonde amesema barakoa hizo zitawasaidia pakubwa wanafunzi hasa wale wanaotoka katika familia maskini.

Kwa upande wao walimu wakuu wa shule hizo wakiongozwa na mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Migwaleni, Mwaringa Ngowa wamesema msaada huo utasaidia wanafunzi kuendeleza masomo bila changamoto.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.