WAKAAZI WATIWI KAUNTI YA KWALE WASITISHA UJENZI WA UA KWENYE MSITU WA KAYA TIWI

Wakaazi wa Tiwi katika kaunti ya Kwale wamesitisha ujenzi wa ua kwenye msitu wa Kaya Tiwi uliokua umeziba barabara ambayo wenyeji wanatumia kwenda kujivinjari katika ufuo wa bahari ya Tiwi.

Ua hilo linasemekana kujengwa na bwenyenye mmoja anayedaiwa kumiliki ardhi ya msitu wa Kaya Tiwi. Aidha wakazi hao wameuharibu ua uliojengwa huku wakisema hawatakubali unyakuzi wa ardhi ya umma.

ikumbukwe miezi 6 iliyopita gavana wa Kwale Salim Mvurya alisimamisha umiliki wa msitu huo baada ya msitu huo kuzungushwa ukutwa hatua inayowashangaza wakaazi wa eneo hilo.

Wakazi hao sasa wanaitaka serikali ya kaunti na serikali ile ya kitaifa kuingilia kati ili kuzuia unyakuzi wa ardhi kwa wenyeji wa kaunti hiyo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.