Wafanyikazi wa kaunti ya Kilifi wa kila ngazi wapigwa marufuku ya kutoka kaunti ya Kilifi

 

Wafanyikazi wa kaunti ya Kilifi wa kila ngazi wamepigwa marufuku na serikali ya kaunti ya Kilifi ya kutoka katika kaunti ya Kilifi.
Agizo hilo limetolewa na katibu wa kaunti ya Kilifi Jefwa Mkare na kushinikiza kuwa hata wale ambao walikuwa wamepewa vibali vya kutoka nje ya kaunti hii pia hawataruhusiwa.
Agizo hilo linamaanisha kuwa wafanyikazi ambao wamekuwa wakifanya kazi kaunti ya Kilifi na kulala katika kaunti ya Mombasa watalazimika kutafuta makao mbadala.
Kwa mujibu wa katibu huyo ni kuwa hakuna gari lolote la kaunti ya Kilifi ambalo litaruhusiwa kutoka nje ya kaunti hii na watakaokiuka agizo hilo walazimika kuwekwa kwenye karantini ya Lazima.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.