Vyombo vya habari vyatakiwa kutoa hamasa ya madhara ya kujiunga na ugaidi

Vyombo vya habari vimetakiwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha jamii kuhusiana na madhara ya kujiunga na makundi ya kigaidi hasa kwa vijana.

Haya yamejiri katika kongamno la wanahabari wa kanda ya pwani ambalo limeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la KECOSCE, lengo kuu likiwa ni kuangazia visa vya utovu wa usalama na namna ya kudumisha amani sio tu kanda ya pwani pekee bali pia taifa la Kenya kwa jumla kwa kudhibiti visa vya kigaidi na hali ya vijana kushawishika kujiunga na makundi ya kigaidi kama lile la Al- Shabaab na itikadi potofu.

Aidha, hali ya ukosefu wa ajira na tamaa ya pesa miongoni mwa vijana imetajwa kuwa baadhi ya changamoto kubwa ambazo zimetajwa kuwakumba vijana nchini na kuwapa msukumo wa kushawishika haraka kujiunga na makundi haramu.

Ni kongamano la siku tatu na limeratibiwa kukamilika kesho Jumatano.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.