Ongezeko la visa vya wizi wa Ng’ombe katika mtaa wa kadzifitseni eneo bunge la Magarini Kaunti ya Kilifi linaendelea kushuhudiwa.
Haya ni kwa mujibu wa Naibu Chifu wa Pumwani Mary Sulubu ambaye anadai kwamba wizi huo umekuwa ukiwatatiza kwani inawasababishia hasara kubwa wafugaji wa eneo hilo.
Hata hivyo, amedokeza kuwa tayari wameanza kuwatia mbaroni baadhi ya washukiwa wakuu na kushtakiwa.
Kwa upande wake, Mzee wa Kijiji hicho Lawrence Katana Mugandi sasa ameitaka serikali kuwaekea kituo cha polisi eneo hilo ili kudhibiti utundu wa wanaojihusisha na visa hivyo.
Katana amedai ufugaji na kilimo ndio uti wao wa mgongo lakini wamekosa usalama wa kutosha.
VISA VYA WIZI WA NG’OMBE WAENDELEA KUSHUHUDIWA KADZIFITSENI
