Visa vya ugaidi changamoto kuu Kenya

Visa vya kigaidi nchini vimetajwa kuwa changamoto kuu ambayo imekuwa ikiathiri pakubwa usalama wa wenyeji wa pwani na taifa la Kenya kupitia mashambulizi ya Mara kwa Mara kutoka kwa makundi ya Kigaidi ya Alshabaab.

Katika taarifa yake kwenye kongamano ambalo linaendelea kwa sasa huko Watamu Kauntu ya Kilifi, mmoja wa wanachama wa bodi ya Kecosce Dr. Othman Mujaid amesema idadi kubwa ya vijana kanda ya pwani wameshawishika pakubwa na kujiingiza katika maswala ya kigaidi na itikadi potofu.

Dr Mujaid amesema hamasisho kwa jumii kupitia vyombo vya habari na wadau katika asasi za usalama kuhusu umuhimu wa kudumisha usalama na amani nchini kutasaidia kwa asilimia kubwa kuvidhibiti visa vya hivyo.

Hata hivyo, amesema iwapo swala la kuwahamasisha vijana dhidi ya kujiunga na makundi ya kigaidi na itikadi kali litakumbatiwa basi hali ya usalama itarejea nchini na vijana kujihusisha na mambo ambayo yanawafaidi maishani.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.