Viongozi wa kidini kaunti ya Kwale wamewataka viongozi wa kisiasa kukoma kupiga siasa za malumbano kwani huenda zikawagawanya wananchi kupitia cheche za matusi wanazozitupiana.
Wakiongozwa na mchungaji Sammy Karuga viongozi hao wamesema kuwa wanasiasa wanaweza kutatua tofauti zao kupitia mazungumzo na wala sio kutukanana katika majukwaa ya kisiasa.
Mchungaji Karuga amesema kuwa ni sharti viongozi wazingatie maadili ya nyadhfa wanazoshikilia ili kuhakikisha kuwa taifa hili linaongozwa vyema.
Mchungaji KARUGA amesema kuna haja ya viongozi wa kidini kupewa jukumu la kuwahamasisha wananchi kuhusu ripoti ya BBi kwani wengi wao hawana ufahamu kilichomo ndani ya ripoti hiyo.