Viongozi kaunti ya Kilifi na pwani kwa Jumla watakiwa kutekeleza miradi ya maendeleo

 

Viongozi wa kisiasa kaunti ya Kilifi na Pwani nzima kwa jumla, wamehimizwa kutekeleza miradi ya maendeleo mashinani badala ya kupiga siasa za mwaka wa 2022.
Baadhi ya vijana mjini Malindi wakiongozwa na Ali Mlanda, wanasema kwa sasa miradi ya maendeleo kaunti ya Kilifi imesimama huku viongozi wakionekana kufanya siasa za uchaguzi mkuu ujao.
Mlanda anasema licha ya miradi tofauti ya maendeleo kutengewa fedha na serikali ya kaunti ya Kilifi, bado haijatekelezwa huku akihofia huenda fedha hizo zilifujwa.
Wakati huo huo, vijana hao wameapa kupinga azma ya baadhi ya wabunge wa Pwani kutaka kuunda chama kipya cha kisiasa.
Wanadai vijana kutoka eneo la Pwani, wamekuwa wakitumiwa na wanasiasa wakati wa kampeni na kisha baadaye kukosa kuangaziwa kwenye miradi ya maendeleo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.